Tume ya taifa ya uchaguzi imewatoa hofu watanzania kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu imejiimarisha kimfumo wa kielektronic kuhakikisha matokeo yote yanayopatikana yanatangazwa ndani ya kipindi kifupi huku ikiahadi kutangaza matokeo ya urais ndani ya siku tano.

Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi inasema katika kipindi hiki hakutakuwa na dosari zozote za kimfumo hasa taarifa za wagombea huku ikijinasibu kuwa kupitia mfumo wake mpya wa kupokea, kuhesabu na kujumlisha matokeo ambao uko kielektronic hakutakuwa na ucheleweshaji wa kutangaza matokeo.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva anasema ni vema vyama vikafuata kanuni na sheria za uchaguzi katika kampeni kwani kushindwa kufanya hivyo nikuilazimisha tume kuchukua hatua kali za kisheria.
 
Katika mahojiano yao na ITV muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa mkutano baina ya viongozi wa dini na tume ya taifa ya uchaguzi baadhi ya viongozi hao wa dini pamoja namasuala mengine walikuwa na haya ya kuzungumza.
 
Kuelekea Agast 22 mwaka huu ambapo ndio filimbi ya kaushia kuanza kampeni za mwaka itakapopulizwa, NEC bado inasisitiza kwa vyama, wafuasi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya nchi.

Post a Comment