LUNDENGA
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya mwenyekiti katika kamati ya kuandaa shindano hilo na badala yake ameacha nafasi hiyo kwa wadau wengine.

Lundenga alitangaza uamuzi huo jana na kudai kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka mingi lakini ataendelea kutoa ushirikiano katika kamati mpya ya shindano hilo.

Uongozi mpya uliotangazwa jana unasomeka hivi: Juma Pinto (mwenyekiti), Lucas Rutta (makamu mwenyekiti), Doris Mollel (katibu mkuu), Jokate Mwegelo (msemaji wa kamati), pamoja na wajumbe 8 ambao ni Hoyce Temu, Mohammed Bawazir, Gladyz Shayo, Magdalena Munisi, Shah Ramadhani, Hamm Hashim, Khalfani Saleh na Ojambi Masaburi.

Hivi karibuni Barala la Sanaa la Taifa (Basata) liliifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, hata ilitumikiaa dhabu hiyo kwa miezi nane kabla ya kufunguliwa.
Takribani miaka mitatu iliyopita, mashindano hayo yaliendeshwa bila ya kufuata taratibu huku kukiwa na lawama lukuki na kamati chini ya Lundenga ililaumiwa kwa kufanya mambo hovyohovyo.

Post a Comment