Je ungependa kuwa na ndoa thabiti ?
Jifunze kugawanya majukumu na mumeo ama mkeo hapo nyumbani.
Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kuwa kugawanya majukumu ya kuwalea watoto kati ya mume na mke kunaimarisha joto la mapenzi nyumbani.

 

Utafiti huo uliofanyika miongoni mwa familia 487 nchini Marekani umebaini kuwa kugawanya majukumu ya kuwalea watoto na mahitaji mengine hapo nyumbani kati ya mume na mke kunasaidia kuimarisha uhusiano baina yao na hivyo pia kupalilia cheche za mahaba kati ya wanandoa.
Katika nyumba ambamo baba na mama wanasaidiana kuwalea watoto kuwalisha kuwavisha kugharamia mahitaji yao utafiti uligundua walikuwa wakishiriki tendo la ndoa kwa kiwango kikubwa zaidi ya wale ambao majukumu yote yaliwachiwa mwanamke.

Hata hivyo waligundua kuwa iwapo majukumu yote aliyatekeleza mume tofauti ilikuwa ndogo sana.
Utafiti huo wenye jina '' 2006 Marital and Relationship Study'', ulitolewa kwa kongamano la wanasaikolojia nchini Marekani na kuonesha kuwa katika ndoa ambazo mwanamke alitelekezewa majukumu na akasalia kuwajibikia asilimia 60% ya majukumu ya kuwalea watoto, wanawake hao hawakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao binafsi katika ndoa.

Hii ni kumaanisha kuwa iwapo mama mzazi ndiye anayewalinda wavisha walisha na kutunga sheria za hapo nyumbani mara nyingi ifikapo wakati wa kuwa mwanamke huwa hawezi kujituma kumridhisha mumewe katika hali ya maisha ya unyumba.
Dr Daniel Carlson, naibu profesa katika chuo kikuu cha Georgia State , anasema;
"jambo ambalo tulishangaa hata nasi ni pale tulipogundua kuwa wanawake walishindwa kutekeleza majukumu ya unyumba wakiwachiwa asilimia kubwa ya majukumu ya malezi ya watoto''
Sasa wasomi hao wameanza kuweka mikakati ya kuendelea na sehemu ya pili ya utafiti wao ilikujibu swali kwanini ndoa zenye wachumba waliogawanya majukumu yana mshiko zaidi haswa ikija katika swala la unyumba na hususan tendo la ndoa ?
Profesa Sir Cary Cooper, wa kitivo cha Biashara cha chuo kikuu cha Manchester anasema kuwa uchunguzi huu unatilia pondo dhana iliyokuwepo tangu miaka ya nyuma kuwa mwanaume mwenye kujali watoto wake anatunukiwa penzi la ziada na mwanamke.

Post a Comment