Msanii wa R&B Marekani Chris Brown siku hizi amekuwa mtu wa kuspend muda mwingi sana na mtoto wake wa kike, kila atakapo kwenda basi na mtoto Royalty yupo nyuma, sio siri mtu wangu ni wazi kuwa Chris Brown anaenjoy sana kuwa na kuitwa baba.
Headlines za Chris Brown time
hii kwenye kurasa za burudani ni ujio wa album yake mpya ambayo
anategemea kuidondosha very soon, kizuri zaidi kuhusu album hii mpya ni
jina aliloipa album hiyo!
Chris Brown kaamua
safari hii awape mashabiki wake kitu tofauti, kitu kitakachowagusa
mioyo ya mashabiki kama vile ambayo mtoto wake kaugusa moyo na maisha
yake… kupitia Twitter page yake Chris alichukua time na kuandika maneno machache yaliosema; “Album yangu mpya itaitwa ‘ROYALTY'”.
Tarehe ya uzinduzi wa album hiyo bado haijafahamika ila kwenye interview moja aliofanya Chris Brown na mtangazaji maarufu wa Radio Ryan Seacrest, Chris alisema hii ni kama zawadi kwa mtoto Royalty ambaye kayabadilisha maisha yake, na aliye mfanya atake kuwa baba bora na mwanaume bora.
Kwa sasa Chris ametoka kutengeneza video ya wimbo wake Liquor siku chache zilizopita na very soon itasogezwa kwetu mtu wangu.
Post a Comment