Maisha ya mshambuliaji wa Liverpool Mario Baloteli ndani ya klabu hiyo yamezidi kuwa magumu baada ya kocha wa timu hiyo Brendan Rogers kumuweka wazi kuwa hana mipango naye kwa msimu huu.
Baloteli ambaye Liverpool ilimsajili msimu uliopita akitokea Ac Milan ya Italia ameshindwa kuonyesha kiwango bora hali ambayo imemlazimu kocha huyo kuingia sokoni kusajili washambuliaji wengine wakiwemo Danny Ings na Christian Benteke.
Hatua aliyofikia Baloteli ni ya kusaka maisha mengine nje ya Anfield baada ya uongozi wa klabu hiyo kuchoshwa na vituko vyake ikiwemo hali ya kutoonyesha juhudi katika mazoeiz na baadhi ya mechi ambazo amepewa nafasi.
Baloteli amekuwa na tabia ya kuendekeza masikhara akiwa mazoezini ambapo hivi karibuni alijifunga mwenyewe katika mechi ya mazoezi huku yeye mwenyewe akisimama katika ya uwanja akicheza .
Post a Comment