Mh Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiagana na watumishia wa tume
hiyo ambapo amesema nchi isiyokuwa na utawala wa sheria ni sawa na watu
wanaoishi katika msitu ambapo mwenye nguvu ndio anayeishi salama.
Aidha rais Kikwete ameonyesha kusikitishwa kwa namna ambavyo
tattizo la migogoro ya ardhi linavyozidi kukua nchini na kusema kuwa
rushwa ni moja ya sababu kubwa inayosababisha hali hiyo kuendelea na
hivyo ni lazima hatua za dhati zichukuliwe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo Mh Bahametom Nyanduga
amesema katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchaguzi mkuu
ni vyema kila mtu na hasa jeshi la polisi kuzingatia utawala wa sheria
ili kuhakisha kuwa uvunjifu wa amani hautokei.
Post a Comment