Akizungumza na waandishi wa habari injinia Leonce Mroso kutoka
kituo cha kuchakata gesi cha madimba kilicho mkoani Mtwara amesema
wamefanikiwa kuifungua gesi kutoka kwenye visima na kusafirishwa kwenye
kituo hicho kwa ajili ya kuchakatwa.
Amebainisha kuwa gesi hiyo kwa sasa imechakatwa na inatarajiwa
kusafirishwa kwenda Dar es Salaam eneo la kinyerezi ili kuunganishwa
kwenye Gridi ya taifa ifikapo tarehe kumi ya mwezi wa tisa ili iweze
kuzalisha umeme.
Hata hivyo amesema gesi hiyo inafaa kutumika majumbani na tayari
utafiti umefanyika katika baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam,
Mtwara na Lindi.
Kituo hicho kinauwezo wa kuchakata gesi futi za ujazo milioni 80
kwa siku lakini lengo ni kuchakata futi za uchazo milioni miambili na 10
kwa siku.
Post a Comment