Mpambano uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania kati ya klabu ya Yanga dhidi ya Azam FC,huu
ni mchezo wa ngao ya hisani umechezwa siku ya Jumamosi ya August 22.
Mchezo huu ambao kila timu imepania kulinda heshima kwani ni mechi
inayowakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Yanga dhidi ya Azam FC ambayo ni mshindi wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia na
kushambuliana kwa zamu, kipindi cha kwanza kilimalizika kila timu
ikienda mapumzikoni bila kuona lango la mwenzake. Kipindi cha pili
kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu. Mchezo uliamuliwa kwa
mikwaju ya penati na Yanga kuibuka na ushindi wa penati 8-7.
Penati za Yanga zilipigwa na Mbuyu
Twite, Amissi Tambwe, Geofrey Mwashiuya, Andrey Coutinho, Haruna
Niyonzima, Deus Kaseke, Kelvin Yondani huku Nadir Haroub akikosa penati
na penati za upande wa Azam FC zilipigwa na Erasto Nyoni, Aggrey Morris,
Himid Mao, John Bocco, Kipre Tchetche, Jean Mugiraneza na Pascal Wawa
na Ame Ally penati zao zilidakwa na Ally Mustapha
Post a Comment