Vyama
vilivyoshindwa kukidhi vigezo ni CCK, TADEA, DP na AFP amabyo imeingia
mitini ambapo akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za tume
baada ya tume kuwatangazia kushindwa kukidhi vigezo mwenyekiti wa CCK Bw
Costantine Akitanda amesema.
Wagombea urais waliowahi mapema asubuhi ni Mh Edward Lowassa
Chadema na Dk Jonh Magufuli wa CCM ambapo kwa nyakati tofauti
waliowasili ofisi hizo za tume wakiwa na wapambe wao wachache na mara
baada ya kuidhinishwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi
wakapata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Wagombea wengine waliofika majira ya mchana ni mgombea urais
kupitia TLP Maxmilian Lyimo na mgombea urais kupitia ACT Bi Anna Mghwira
ambaye ni mwanamke pekee aliyeingia katika kinyang'anyiro hicho kwa
uchaguzi wa mwaka huu ambaye chama chake kimemteua siku chache kabla ya
ukomo wa kurudisha fomu lakini pia kimevunja rekodi kwa kutafuta
wadhamini kwa siku moja na hatimaye kukidhi vigezo vya tume.
Katika zoezi hilo vituko vya hapa na pale navyo havikukosekana
katika ofisi za tume ya uchaguzi baada ya mgombea urais kupitia tiketi
ya chauma kufika katika ofisi hizo na kujikuta akiwa hana picha hivyo
kulazimika kurudi nyumbani kuzifuata huku akirudi dakika za majeruhi
lakini pia wapo walioelezea changamoto walizokumbana nazo wakati wa
kutafuta wadhamini.
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji Damian Lubuva
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha zoezi hilo
ametolea ufafanuzi baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na walioshindwa
kukidhi vigezo huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi katika eneo hilo
la tume ya uchaguzi.
Post a Comment