Jumapili iliyopita rapa Kanye West alipanda kwenye Jukwaa la
MTV/VMAs kupokea tuzo ya heshima ya mafanikio katika maisha yake ya
muziki (Lifetime achievement award) na kuiambia dunia kuwa atagombea
urais wa Marekani mwaka 2020.
Rapa huyo alitoa tangazo hilo kubwa baada ya kupokea tuzo hiyo
aliyokabidhiwa na Tailor Swift, ambapo aliongea mambo mbalimbali
aliyopitia katika maisha yake ikiwa ni pamoja na matukio ya kuzomewa
pale alipokuwa akijaribu katika maisha mengine.
“Kama ningekuwa na mtoto katika kipindi kile ningeenda kwenda
jukwaani na kunyakua Mic kutoka kwa mtu mwingine?” Alisema akikumbushia
tukio alilofanya la kumpokokonya Tailor Swift Mic miaka kadhaa iliyopita
kwenye tuzo hizo.
“Unajua, kesho nyakati kama hizi, itakuwa kitu kingine kabisa,
tamasha fulani, kitu kama hicho. Hata ile imepita, lakini madhara
yaliyokuwa na watu yamebaki. Kama mgekuwa mgeweza kuhisi hadi wakati
huu, nimeamua, mwaka 2020 nitagombea urais,” alisema Kanye West.
Post a Comment