Kundi
la watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia na kuibomoa nyumba
ya mgombea ubunge wa chama cha wananchi CUF jimbo jipya la nanyamba
wilaya ya mtwara vijijini, twahiri saidi baada ya kushindwa kurudisha
fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku simu zake za mkononi
zikiwa hazipatikani.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya viongozi wa chama hicho na
wanachi wa jimbo la Nanyamba wamesema mazingira aliyotoweka mgombea huyo
yanaonyesha wazi kuna mchezo mchafu umefanywa ili kutoa fursa kwa
mgombea wa CCM Abdallah Chikota kupita bila kupingwa katika jimbo
hilo.
Akizungumzia tukio hilo katibu kata wa CUF kata ya Milango Minne
eneo analotoka mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na mgombea
huyo ilikuwa majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa msimamizi
wa uchaguzi.
Hata hivyo anasema majibu ya mgombea huyo yalionyesha wazi kuna
jambo baada ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia kwenye
kinyang’anyiri cha uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi
kumpa shilingi milioni 30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya
hivyo na baada ya maneno hayo simu zake hazikuweza kupatikana mpaka muda
huu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya maji wa nanyamba oscar
ng’itu ambaye aliongozana na mkuu wa kituo cha polisi nanyamba
alitembelea nyumba iliyobomolewa na kutoa agizo kwa wananchi kuwataja
watu waliyohusika na tukio hilo vinginevyo mkono wa sheria utachukua
mkondo wake.
Post a Comment