Aliyekuwa Waziri mkuu wa Serikiali ya awamu ya Tatu Fredrick Sumaye ametangaza rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema  na kuungana  na Waziri mkuu wa awamu ya nne Edward lowassa.
 
 Akizungumza na waandishi wa Habari leo  mchana Jijini Dar es salaam ,Sumaye amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na uvunjaji wa kununi  ndani  ya  CCM  ikiwemo katika harakati za kumteua mgombea wa Urais kwa upande wa CCM akidai mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete alitumia ubabe katika kuwaingiza watu wake tano bora.
Habari  kwa  Kina  itakuijia  hivi  punde. 
 


Post a Comment