Utafiti umeeleza kuwa Watu
wanaofanya kazi kwa saa nyingi wako hatarini kupata kiharusi,utafiti huo
ulifanywa kwa zaidi ya watu laki tano.
takwimu zilizochapishwa
kwenye jarida la kitabibu,Lancet, linaonyesha upo uwezekano wa ongezeko
la hatari ya ugonjwa huo kwa watu wanaofanya kazi zaidi ya muda wa
kawaida.Wataalam wanasema watu wanaofanya kazi kwa saa nyingi zaidi wawe na utaratibu wa kupima kiwango cha msukumo wa damu.
Dokta Mika Kivimaki , kutoka Chuo cha jijni London.
Wataalamu wanasema kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida na kukaa kwa muda mrefu ni mbaya kwa afya na ongezeko la hatari ya kupata kiharusi.
Daktari Kivimaki ameuambia Mtandao wa Habari wa BBC kuwa watu wanapaswa kuwa makini na afya zao,kuangalia mtindo wao wa maisha na kuhakikisha wanapima vipimo vya damu kuepuka shinikizo la damu.
Post a Comment