Mchezaji wa Everton ambaye ni raia wa Jamhuri ya Ireland nyota wa kabumbu Darron Gibson, amepigwa faini kwa kusababisha ajali na kukimbia; ajali iliyomuacha muendesha baisikeli na majeraha mwilini mwake.
Kiungo huyo mwenye miaka ishirini na saba aliwekwa kizuizini mwanzoni mwa wiki hii baada ya polisi kupokea taarifa za tukio la mwendesha baisikeli aliyegongwa na gari ambayo pia ilikwenda kugonga pampu ya kujaziamafuta kwenye kituo kimoja cha mafuta.Gibson anatuhumiwa kuendesha gari akiwa amelewa ,na kuhusika kwenye tukio lingine awali huko Altrincham, Manchester.
Inaelezwa zaidi kwamba mchezaji nyota huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari aina ya Nissan Skyline GT-R Nismo nyeusi na ajali hiyo imetokea mita chache kutoka kwenye makazi yake .Polisi wa Greater Manchester wamesema kwamba Gibson ameshtakiwa kwa kuendesha bila uangalifu na bila kujali,kuendesha akiwa amekunywa pombe na pia kushindwa kusimama baada ya ajali hiyo.
Gibson mzaliwa wa Londonderry alianza kuonesha cheche zake katika klabu
ya Manchester United kabla ya kujiunga na klabu ya Everton mnamo mwaka
2012 kwa gharama ya paundi milioni moja. Mchezaji huyo anaendelea kupona
kutokana na ajali ya awali aliyoipata uwanjanai.Naye msemaji wa klabu
hiyo Everton amekataa kuzungumza lolote kuhusiana na tukio hilo .
Post a Comment