Kampuni ya vifaa vya michezo ya Kijerumani ADIDAS
ambayo ni wadhamini wa vilabu kadhaa vya soka barani Ulaya imeandaa
mashindano maalum ya kutangaza jezi mpya za timu walizozidhamini.
Mashindano hayo ni ya tofauti na sio kama tuliyoyazoea kwani yalikuwa
yakihusisha wachezaji wawili wawili.
Wachezaji wa vilabu vya Man United, Chelsea, AC Milan, Bayern Munich na Real Madrid kila klabu ilitoa wachezaji wawili kushiriki katika mashindano ambayo ADIDAS waliyapa jina la be the difference ilikuwa kwa ajili ya kuzindua jezi za tatu za timu zilizodhaminiwa na Adidas.
Wachezaji waliyohudhuria mashindano hayo yaliyofanyika Marseille Ufaransa ni Ashley Young , Morgan Schneiderlin wa Man United, Victor Moses, Cesar Azpilicueta wa Chelsea na Riccardo Montolivo na Philippe Mexes wa klabu ya AC Milan.
Post a Comment