Mshambuliaji wa Liverpool Mario
Balotelli amewasili katika kilabu ya AC Milan ili kufanyiwa ukaguzi wa
matibabu kabla ya kurudi katika timu hiyo kwa mkopo wa mwaka mmoja
kilabu hiyo imetangaza.
Mshambuliaji huyo wa Italy mwenye umri wa miaka 25,huenda akacheza mechi yake ya kwanza katika ligi ya Serie A dhidi ya mahasimu wao Empoli siku ya jumamaosi.
Aliifungia Liverpool bao moja pekee baada ya kuhamia Liverpool kutoka Milan kwa pauni milioni 16 mnamo mwezi Agosti mwaka 2014.
Aliwachwa nje katika mechi za kirafiki za kikosi cha Liverpool huko mashariki na Australia na amekuwa akifanya mazoezi mbali na kikosi cha kwanza.
Liverpool imewasajili Christian Benteke,Roberto Firmino na Danny Ings,huku Divock Origi akiwasili.
Post a Comment