Klabu ya Manchester United bado inasaka nyota kadhaa watakaojiunga na kikosi chao ili kuweza kuongeza nguvu na kucheza kwa kiwango cha juu. Man United ambayo kwa hivi karibuni ilimkosa Pedro Rodriguez baada ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho kumpigia simu na kumshawishi ajiungea na Chelsea.
Sasa Man United wamerudi tena katika klabu ya FC Barcelona
ila safari hii wanahitaji kumsajili nyota ambaye wengi wanaamini hawezi
kuuzwa kipindi hiki. Inaripotiwa na vyombo vingi vya habari Uingereza
kuwa Man United wanataka kumsajili Neymar na wametenga kiasi cha pound milioni 240 ili kumpata nyota huyo.
Stori zilizopo kwa sasa FC Barcelona wanajiandaa kumpatia Neymar mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya pound milioni 182, Mkataba ambao utamuweka Neymar Nou Camp hadi mwaka 2023. Mkataba wa Neymar wa sasa utamalizika mwaka 2018.
Post a Comment