Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema amechoshwa na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima hapa nchi kwa kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na serilkali bila ya wao kupata faida yoyote.
Lowassa
alisema punde atakapochaguliwa kuongaza nchi kitu kikubwa
atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao
kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.
Lowasa
ameyasema hayo leo wilayani Mufindi alipofanya mkutano wa hadhara wa
kampeni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, mjini Mafinga.
Lowassa
alisema watu wamekuwa wakizungumza kuwa CCM ni wezi wa kura kwasababu
ni wajanja sana katika kufanya michezo michafu katika chaguzi na maneno
hayo si yakuyabeza wala kuyafumbia macho.
“Mimi
nataka kila mtu akihifazi vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura)
na siku ya kupiga kura ikifika nawaomba wanawake na wanaume wajitokeze
kwenda kupiga kura ila wakina baba nawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi
ya kuzilinda kura zenu” alisema Lowassa
Katika
mkutano huo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai alipanda jukwaani
na kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chadema,
William Mungai ambaye ni mtoto wake.
Mungai
aliwahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na aliweza kuteuliwa
nafasi mbalimbali za uwaziri ikiwamo Wizara ya Kilimo, Mambo ya Ndani na
Wizara ya Elimu.
Mungai
alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William Mungai kwa
sababu mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo hakuweza kuongoza
kama alivyofanya yeye.
Post a Comment