Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia mwenye asili ya Ghana anayeichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza Mario Balotelli
ambaye amezoeleka kuingia katika headlines mbalimbali kuhusiana na
tabia yake ya ukorofi na vituko vyake safari kaingia tena katika
headlines ila sio kwa ukorofi au utukukutu.
Hii ni good news kwa mashabiki watoto wa
mshambuliaji huyo kwani amekuja na Brand ya viatu vya mpira wa miguu na
mipira, vifaa hivyo vitakuwa vinapatikana kwa ajili ya watoto, huku
vikiwa vinastahili ya kipekee tofauti na tulivyozoea.
Brand hiyo ya vifaa vya michezo ya Balotelli imetengenezwa na kampuni maarufu ya Kijerumani kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo PUMA, vifaa hivyo vinastahili kama ya manyoya au nywele kama ambavyo Balotelli amekuwa akinyoa stahili ya kiduku katika kichwani kwake.
Post a Comment