Baada ya jana kufanyika droo ya
makundi ya klabu bingwa barani Ulaya, mashabiki wa soka watapata fursa
ya kushuhudia baadhi ya historia zikijirudia huku zingine mpya
zikiandikwa.
Arsenal kwa mara ya tatu katika misimu minne, itavaana na Bayern Munich baada ya kupangwa kundi moja.
Wakati
hayo yakijiri, mchezaji mpya wa Manchester Utd Memphis Depay atapata
fursa ya kupambana na timu yake ya awali ya PSV Eindhoven ya uholanzi
baada ya timu hizo kupangwa kundi moja.
Na ligi kuu ya Hispania La
liga, pia mwaka huu imeweka historia baada ya mwaka huu kuingiza timu
tano katika hatua hiyo ya makundi, jambo ambalo halikuwahi kutokea hapo
awali.
Timu hizo ni Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid, Valencia pamoja na Sevilla.
Post a Comment