First Lady wa Young Money, Nicki Minaj ametengeneza rasmi uadui
na Miley Cyrus baada ya kumponda wakati anapokea tuzo ya video bora ya
hip hop (Anaconda) kwenye jukwaa la MTV/VMAs 2015, Jumapili, Agosti 30.
Nicki alimrushia maneno Miley Cyrus ambaye alikuwa mshereheshaji
katika tuzo hizo ikiwa ni majibu yake kwa Miley aliyetoa maoni juu ya
bifu la rapa huyo wa kike na Tailor Swift hivi karibuni alipofanya
mahojiano na The New York Times akidai kuwa majibu ya Nicki kwa Swift
hayakuwa ya upole na ukarimu.
Akiwa jukwaani, Nicki alianza kwa kuwashukuru mashabiki wake kwa
kumuwezesha kushinda tuzo hiyo na mwisho akamjibu Miley kwa kumtaja jina
huku akitumia maneno makali.
“Back to this b***h that had a lot to say about me the other day in
the press. Miley, what’s good?,” aliuliza Nicki na kuwaacha watu midomo
wazi.
Miley naye alirukia na kujibu haraka akidai vyombo vya habari
vinapika mambo huku akimpongeza Nicki kwa ushindi wake kama ishara ya
kuua kiaina kinachoendelea.
“Hey, we’re all in this industry, we all do interviews and we all
know how they manipulate s**t. Nicki, congratulations,” alijibu Miley
Cyrus.
Post a Comment