MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imekipa onyo kali kituo TBC1 kwa kosa la kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na UKAWA.
Hukumu
hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya
utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Bugoya
alisema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya
mwaka 2005 pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kufanya
upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye kipindi.
Alidai
katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu
majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu, katika kipingele cha uchambuzi
wa magazeti mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku
akiruka kusoma habari kuu husika.
Alisema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanganya umma jambo ambalo amedai ni kosa.
Bugoya
alitaja makosa hayo kuwa ni wakati mtangazaji huyo alipokuwa anasoma
Gazati la Majira ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni “CCM yazidi kuwaumbua wanaomfuata lowassa” wakati habari kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema “Mbeya kwafurika”, huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.
Alisema
mtangazaji huyo pia alifanya kosa lingine kama hilo pia wakati akisoma
Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni “Mbalawa atoa sheria ya mitandao” ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile “Mafuriko Mbeya” na sio aliyokuwa anaisoma yeye.
Alisema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana.
Mkurugenzi
huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo
hakufanya kosa kwakuwa alikuwa hajaridhika na taarifa zilizokuwa
zimeandikwa kwenye magazeti hayo.
Sanjari
na hayo Mshana alizidi kujitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo
asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti
hayo tayari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima
wa kusomwa.
Bugoya
alisema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo
hicho kilikiuka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka
vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na
upendeleo wowote.
Post a Comment