Najua nina watu wangu wanaopenda stori
za siasa sasa stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa aliyekuwa
mbunge wa viti maalumu kupitia CCM Ester Bulaya pamoja anaonekana kwenye
headlines mpya za Chadema baada ya kuhamia chama hicho anasema
hakutegemea kuhama chama cha Mapinduzi (CCM).
‘Kuhama inatokea na mazingira
lakini mimi sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuhamia Chadema lakini
mienendo, tabia, future ya kuwatumikia wananchi ilikuwa imepotea mimi
nimekulia CCM na am proud for that wamenilea lakini walinilea kwenye
misingi ya uwazi na ukweli kile walichonifunza nikitaka kukitumia
hawataki sasa kama kuna wengine kile nilichofundishwa huku wao
wanakiaminia kutoka moyoni na midomo mwao niende kujiunga nao lakini
wote tukiwa na ndoto za kuwatumikia wananchi’ -Ester Bulaya‘Unajua kuna tofauti ya utumishi na mtu kufikiri utumishi ni cheo wanaofikiri ubunge ni cheo ni wale ambao hawatimizi wajibu wao wanataka ubunge kutaka madaraka Fulani, mimi ni mtumishi naenda kuwatumikia wananchi mabosi wangu ni wananchi ukiwa unadhani ya kwamba ubunge ni cheo utavimba kichwa na utashindwa kutimiza wajibu wako, bunge bosi wake ni wananchi‘ – Ester Bulaya.
Post a Comment