Marais
wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, wanatarajiwa kushiriki
kwenye ufunguzi wa kampeni za kumnadi mgombea wa urais wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli Jumapili, jijini Dar es Salaam.
Pia
uzinduzi huo unatarajiwa kupambwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa
kizazi kipya wakiongozwa na Nasiib Abdul (Diamond) na bendi mbalimbali
ikiwamo ya Tanzania One Theatre (TOT).
Kadhalika,
wamo marais wastaafu wa Zanzibar, mawaziri wakuu wastaafu, viongozi
wakuu wastaafu wa CCM na viongozi wa serikali, makada kutoka mikoa
mbalimbali nchini na wananchi wanatarajiwa kuhudhuria.
Habari
za uhakika kutoka vyanzo vyetu ndani ya CCM zinaeleza kuwa baada ya
kampeni hizo kuzinduliwa jijini Dar es Salaam, ziara ya kumnadi
itaelekea mikoa ya kusini.
Mikoa hiyo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwamba ratiba hiyo itafuata hadi kumalizika nchi nzima.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (pichani), alipoulizwa, alisema ratiba kamili itatolewa baadaye kwa vyombo vya habari.
Kuhusu
wageni mbalimbali wa heshima ambao wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo
alisema hafahamu na kwamba mgeni rasmi ni mgombea mwenyewe ni Dk. John
Magufuli.
Nape
akizungumzia ilani ya uchaguzi ya chama hicho, alisema inatarajiwa
kuzinduliwa siku ya kuzindua kampeni.Mpekuzi jana ilishuhudia uwanja wa
Jangwani ukifanyiwa usafi.
Magari ya ya kubeba mizigo yalionekana yakisomba taka na udogo uliokuwa ukichimbwa eneo hilo.
Post a Comment