Newcastle United ilijitahidi nakuwadhibiti wenyeji wao Manchester United katika mechi ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza iliyomalizika muda mchache uliopita uwanjani Old Trafford.
Newcastle ilijifurukuta na kuvunja rekodi ya kushinda mechi zote msimu huu iliyokuwa imewekwa na Man united.
Chini ya mkufunzi Steve MClaren, Newcastle United ilikaza buti na kuwanyima washambuliaji wa manchester fursa ya kushambulia lango lao.
Aidha vijana hao wa Mclaren walijizolea alama yao ya pili msimu huu.

Vijana wa kocha Louis van Gaal hata hivyo walitamaushwa na kauli ya refarii aliyepuliza kipenga na kuashiria bao la mshambulizi Wayne Rooney kuwa halikufaa na kuwa alikuwa ameotea
Nusura Newcastle wafunge bao la kwanza kupitia mkwaju wa Aleksander Mitrovic uliogonga mwamba wa lango baada ya kuwapita walinzi na kipa wa manchester.
Mshambulizi huyo wa Serbia aliwaacha walinzi wa manchester hoi.
Muda mchache baadaye nipe nikupe kati ya washambulizi wa Manchester nusura izae matunda isipokuwa tu juhudi za Tim Krul wa Newcastle aliyezima kombora la Javier Hernandez.
Mashambulizi hayakuishia hapo, vijana wa van Gaal waliendelea kushambulia lango la Newcastle hadi dakika ya mwisho dakika tano za ziada Chris Smalling alipogonga mchuma wa
Newcastle sekunde chache tu kabla ya mechi hiyo kumalizika.
Man Utd 0 - 0 Newcastle
Mpira umekwisha
90:30 Muda wa kawaida umekwisha hapa Old Trafford na hakuna aliyeona lango la mwenziwe matokeo bado.

Post a Comment