Wanawake
kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika
ukumbi wa Milenium Tower katika mkutano wa baraza la wanawake wa Chadema
ambao mgeni rasm ni mgombea wa urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa ambaye
amewataka wanawake kushiriki ipasavyo katika kuleta mabadiliko.
Mh Lowassa aliyeambatana na viongozi wa juu wa chama hicho amesema
wanawake wana mchango mkubwa wa kufanikisha ndoto za watanzania za
kupata mabadiliko ya kweli.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa UKAWA akiwemo mwenyekiti wa
Chadema Mh Freeman Mbowe amewataka viongozi wa UKAWA kote nchini
kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa nafasi ya kutoa mchango wao ipasavyo.
Awali mke wa mgombea urais kupitia UKAWA mama Regna Lowassa
amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kupokea
mabadiliko sambamba na kujitokeza kupiga kura na kuhakikisha mabadiliko
yanapatikana kwa amani na yanasaidia kupunguza makali ya maisha
Post a Comment