SIKU mbili baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kumvua Ukamanda Mkuu, mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, uamuzi huo umepokewa tofauti na mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Edward Lowassa.
Tamko
la UVCCM ambalo lilitolewa na Katibu Mkuu wa umoja huo,Sixtus Mapunda,
lilisema wamefikia uamuzi huo kutokana na tabia, mwenendo wa Mzee
Kingunge aliounesha hivi karibuni tofauti na maadili pamoja na taratibu
za CCM.
Umoja huo ulipendekeza vikao vya CCM, kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.
Bw.
Lowassa ambaye pia ni mgombea urais anayeviwakilisha vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), alisema CCM itapata laana kama
itaridhia kuondolewa kwa Mzee Kingunge.
Akiwahutubia
mamia ya wafuasi wa UKAWA katika Viwanja vya Kibandamaiti, Mjini
Zanzibar, jana ambako alikwenda kutambulishwa na kutafuta wadhamini, Bw.
Lowassa alisema Mzee Kingunge ni mmoja kati ya wazee muhimu ndani ya
CCM.
"Nasikitika sana kwa hatua kali alizochukuliwa Mzee Kingunge, kama isingekuwa yeye, CCM isingefika hapo ilipo, watapata laana," alisema.
Mapokezi yake
Lowassa
aliwasili Zanzibar jana asubuhi akitokea jijini Mwanza kwandege ya
kukodi akiwa na viongozi wengine wa UKAWA pamoja na mgombea mwenza, Bw.
Juma Duni Haji.
Baada
ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, msafara huo
ulipokewa na Katibu Mkuu wa CUF Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa
Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Akihutubia
mkutano huo, Lowassa aliwaambia Wazanzibar kuwa atahakikisha
anazingatia taratibu za kisheria ili Masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara ya
Kiislamu (Uamsho) wanaoshikiliwa katika mahabusu jijini Dar es Salaam,
wanapata haki zao.
Ahadi hiyo ya Lowassa ilisababisha umati huo kulipuka kwa furaha na vifijo huku ukimuita `Rais, Rais, Rais.
Alisema kwa mara zote alizokwenda Zanzibar, hajawahi kushuhudia umati mkubwa kama aliouona jana.
Lowassa
alisema amekwenda Zanzibar kuomba dhamana ya wananchi na kurudia kauli
yake kwamba anawania urais kwa kuwa anauchukia umaskini.
“Nataka
kuwahakikishia Watanzania popote kwamba mabadiliko yataletwa na vyama
vya upinzani. Nimetembea sehemu mbalimbali nimeona wananchi wanataka
mabadadiliko ya uongozi,” alisema.
Kuhusu
Katiba, alisema yeye ni muumini wa Serikali Tatu zitakazosaidia
kuimarisha Muungano na kwamba msimamo wake huo aliouonyesha tangu miaka
ya 90 wakati wa harakati za kundi la G55.
Alisema suala hilo litafafanuliwa vizuri wakati wa uzinduzi wa ilani ya uchaguzi Jumamosi wiki hii na wakati wa kampeni.
Hata hivyo, Lowassa alisema njia ya kuiondoa CCM madarakani, ni kwa kupiga kura na wananchi wajiandae pia kulinda kura.
Masheikh waliofungwa
Alisema
Masheikh mkoani Mwanza walimwomba azungumzie jambo hilo na kwamba
atakachofanya atakapoingia madarakani, atazingatia taratibu za kisheria
kufuatilia stahili zao.
Post a Comment