Miziki inayowekwa kwenye mitandao
sasa itaanza kuorodheshwa kulingana na umri wa watu ambao wataruhiwa
kutizana sawa na jinsi filamu zinavyoorodheshwa
Makampuni ya muziki ya Sony, Universal na Warner yatatuma video kwenda kwa bodi ya filamu ya Uingereza kabla video hizijawekwa kwenye mitandao ya You Tube na Vevo.
Kati ya video 132 zilizowasilishwa kwa bodi hiyo 56 ziliorodheshwa katika kiwango cha 12 huku 53 zikiorodheshwa kiwango cha 15.
Viwango hivyo vitatolewa kwa video za muziki ambazo hutolewa nchini Uingereza.
Wasanii wa kimataifa ambao huzua utata kupitia kwa video zao kama Rihanna na video yake ya Better Have My Money hawataathiriwa.
Serikali inasema kuwa mpango huo utawalinda watoto kutokana na kutizama video zisizostahili kupitia kwa mitandao.
Post a Comment