Tanzania inatarajia kuwa wenyeji wa fainali za
Afrika za soka kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika
mwaka 2019.
Akizungumza na BBC leo jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho la soka la
Tanzania (Tff) Jamal Emmily Malinzi amethibitisha kuwa Tanzania watakuwa
wenyeji wa fainali hizo .
Amesema Tff kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania walituma maombi katika
shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuomba kuwa wenyeji wa fainali hizo na
hatimaye Caf imeridhia Tanzania kuwa wenyeji mashindano hayo.
Na shirikisho la soka Tanzania (Tff) likiwa katika mikakati ya maandalizi ya
fainali hizo, Rais huyo amewataka wadau mbalimbali wa soka nchini Tanzania
yakiwemo mashirika ya watu binafsi , sekta binafs i kujitokeza na kutoa
michango ya fedha na vifaa kwa lengo la kufanikisha fainali hizo na hatimaye
kuweza kujitangaza kisoka kupitia fainali za afrika kwa vijana walio chini ya
umri wa miaka 17.
Post a Comment