Mgombea
urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli
ameonesha kushangazwa na miradi kadhaa ya maendeleo nchini kukwama
katika sekta mbalimbali huku fedha zikiwa zimeshatolewa jambo
linalowafanya watanzania kuichukia serikali yao na kusababisha mianya ya
rushwa na hivyo kuwataka watanzania wampe ridhaa ya kuliongoza taifa
ili aweze kuisimamia miradi hiyo kikamilifu na kuleta maendeleo nchini
lakini pia kubana fursa za ubadhirifu zinazosababisha kero kubwa kwa
wananchi wa hali ya nchini.
Akitokea mkoani Rukwa kuelekea mkoani Mbeya mgombea huyo wa kiti
cha urais kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufulia ambaye
ameonekana kuungwa mkono na makundi mbalimbali wakiwemo walemavu na
viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini amezungumza na maelfu ya wakazi
wa Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia amewaambia watanzania kupitia
wakazi hao kuwa katika utendaji wake wa miaka 20 serikalini hakuwai
kuonywa ama kufukuzwa na ametekeleza majukumu yake kwa weledi na
uadilifu mkubwa kutokana na kiu yake ya kutaka kuona watanzania wanapata
maendeleo ya kweli hasa wale wananchi wa kipato cha chini.
Aidha Dr Magufuli amesema endpo atapata ridhaa ya watanzania
kuliongoza taifa wananchi watashangazwa na namna nchi itakavyopiga hatua
mbele za kimaendeleo kwa kuwabana wale wote wanaopaswa kutekeleza
miradi ya maendeleo kwa kuwa nao maeneo ya kazi jambo litakalosaidia
kuzuia pia ubadhirifu.
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi Mh William Lukuvi
amemfananisha Dr Magufuli kama tingatinga lenye uwezo wa kung’oa magugu
yote katika sekta mbalimbali kiwemo kero za rushwa, ubadhirifu na
urasimu unaofanya maendeleo kurudi nyuma.
Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara yake mkoani Mbeya baada
ya kuzungumza na wakazi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Tunduma ambapo
mamia ya wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kumlaki na kumsikiliza
ambapo imeelezwa amevunja historia ya mikutano mikubwa iliyowahi
kufanyika katika maeneo hayo.
Post a Comment