Kocha Louis van Gaal ameendelea kusafisha timu kwa kuuza wachezaji au
kuwatoa kwa mkopo. Baada ya mchana wa leo kumtoa kwa mkopo Januzaj,
jioni hii klabu ya Manchester United imemuuza mshambuliaji wake Javier
“Chicharito” Hernandez.
![](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_7772.jpg?w=620)
Mshambuliaji
wa Mexico ameuzwa kwenda klabu ya Bayer Leverkusen na amesaini mkataba
wa miaka 3 na klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Ujerumani.
![](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_7775.jpg?w=620)
Chicharito
aliyejiunga na United kutoka klabu ya Guadalajara kwa ada ya £6.9m
mwaka 2010, ameuzwa kwenda Leverkusen kwa ada isiyopungua kiasi cha
£8.75 million
Post a Comment