Baada ya kuweka headlines siku ya jana kwa kufanya collabo na superstaa kutoka Marekani Ne-Yo, staa wa Bongo Flava Diamond Platnumz yupo njiani kuelekea South Africa kufanya ile collabo tuliyoisikia kwa muda mrefu sana na Mafikizolo.
Wimbo unaitwa “Tell Every One” ambao ni sehemu ya kampeni ya The Global Goals, kampeni kubwa ya dunia inayolega kutokomeza njaa, umasikini maradhi na matatizo mengine.
Mafikizolo tayari washaingiza sauti zao kali kwenye ngoma hio na sasa ni zamu ya mtu wetu anayeiwakilisha Tanzania Diamond Platnumz kunogesha ngoma hiyo. Kizuri zaidi ni kwamba hata mchezaji mpira wa Real Madridn, Gareth Bale ni sehemu ya kampeni hiyo kubwa duniani.
Post a Comment