Mchezaji mpya wa Chelsea Pedro
amefichua kwamba alikataa kujiunga na timu zote mbili za Manchester na
badala yake kujiunga na Chelsea.
Amesema kuwa alikataa ombi la kujiunga na timu hizo za Manchester huku akisema kuwa ushirikiano wa Jose Mourinho,Cess Fabregas na makao ya Stamford bridge ni baadhi ya vivutio vilivyomvutia.
Kilabu ya Manchester United ilikuwa kifua mbele katika kutafuta saini ya Pedro lakini ni Chelsea ilioharakisha uhamisho huo huku Mourinho na Fabregas wakihusika pakubwa katika kumrai ,mchezaji huyo.
Post a Comment