Inafahamika
kuwa viongozi wengi wa Afrika wanapenda kujilimbikizia mali na kukaa
madarakani ili kuendelea kuongoza nchi zao, wengine husababisha hata
nchi kuingia kwenya machafuko ya kisiasa.
Kuna hii ya Rais wa Gabon imenifikia mtu wangu, yeye amewaahidi vijana wa nchi yake kuwapa urithi wa mali zake.
Ali Bongo Ondimba amesema mali zote alizopewa na baba yake mzazi Omar Bongo ambaye alitawala Taifa hilo kwa miaka 41 atawapa vijana wa Gabon ikiwemo kuuza majengo mawili ya kifahari yaliyopo Ufaransa.
Kwenye
ahadi nyingine ni kwamba jengo moja la kifahari lililoko katika mji mkuu
wa Gabon litabadilishwa na kuwa chuo kikuu cha Umma.
Maamuzi
ya Rais huyo yamekuja wakati wanasheria wa Ufaransa wakiwa wanachunguza
mamilioni ya mali za familia ya Rais huyo zilizotumika kununua na
kujenga majumba ya kifahari nchini humo.
Post a Comment