Licha ya sheria hizo mbili zilizopitishwa na bunge mapema april
mosi huku zikitajwa kuwa ni tata na kandamizi kwa watumiaji wa mitandao ,
serikali inasema sasa ni rasm utekelezaji wake sept mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa sheria hiyo ya mitandao ya mwaka 2015, inatoa nafasi
finyu kwa mtumiaji wa mitandao huku ikipiga marufuku, kutuma jumbe
zisizo thibitishwa, picha za utupu, jumbe zozote zenye lengo la
kudhalilisha ikiwa ni pamoja na taarifa zenye lengo la kuposha umma,
watumaji wanasema wamejipanga kutekeleza.
Lakini kwa mujibu wa mtaalam wa masuala ya ICT kutoka chuo kikuu
cha Dar es Salaam Bw Moses Ismail anasema licha ya sheria hiyo kali ni
dhahili serikali italazimika kutumia nguvu kubwa kwani teknolojia haina
mipaka.
Sheria hizo mbili zilizopitishwa bila baraka za kambi rasm ya
upinzani bungeni, serikali inasema Tanzania si nchi ya kwanza kuwa na
sheria kama hizi, kwani pamoja na mambo mengi itasaidia kupunguza nyingi
zinazotokana na matumizi hasi ya teknolojia.
Wakati utekelezaji wa sheria hizo ukianza mapema septemba mosi,
baadhi ya taasisi za kisheria nchini ziko mafichoni sasa zikijipanga
kuzipinga sheria hizo mbili mahakamani kwa madai si rafiki kwa watumiaji
wa mitandao.
Post a Comment