Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi taifa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Dr Jakaya Mrisho Kikwete amesema mchakato wa uteuzi wa mgombea wa
nafasi ya urais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli umedhihirisha kuwa
chama hicho hakiteuwi kada ama mwanachama yeyote kutokana na fedha zake
na kwamba uteuzi wake umetokana na mapenzi ya mungu kwa Tanzania kumpata
mtu atakayesimamia kwa dhati rasilimali za taifa na kuwatumikia
wanyonge na asiyeyumbishwa na rushwa.
Akizungumza na wanaccm mkoa wa Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama
cha mapinduzi taifa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya
Mrisho Kikwete amewahakkishia wanaccm wote nchini kuwa chama hicho kina
mgombea mzuri tena mzuri sana katika kila hali iwe na ya ucha mungu,
uwajibikaji na uchapakazi kwa kuzingatia misingi ya haki na hana
kigugumizi katika utendaji wake na kwamba ni mpango wa mungu Tanzania
kumpata kiongozi mwadilifu atakayesimamia uwajibikaji na uadilifu na
kwamba ni mtu asiyejikweza na kwamba ni mgombea wa sampuli nyingine.
Akielezea sifa za Dr John Pombe Magufuli mwenyekiti huyo wa CCM
taifa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho
Kikwete amesema Dr Magufuli anachukia sana uzembe, rushwa na ubabaishaji
lakini pia usawa wa kijinsia na ndo maana akamteuwa mgombea mweza kuwa
mwanamke.
Mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli
akizungumza na wanaccm hao wa mkoa wa Dar es Salaam amesema Tanzania ni
nchi ya amani ambayo inapaswa kuendelezwa kwa misingi ya amani bila
ukabila na ukanda wala ubaguzi wa aina yeyote na kuwataka watanzania
kuendelea kuwa wamoja na kuwahakikishia watanzania kuwa anatosha katika
kutatua kero mbalimbali za mtanzania wa kawaida na makundi mbalimbali.
Awali, akizungumza na wanaccm mkoa wa Dar es Salaam, mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM
mikoa Ramadhani Madabida amesema mkutano huo ni wa kwanza tangu
kumalizika kwa vikao vya uchujaji wa wagombea katika ngazi zote
vilivyoongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Dr Jakaya Kikwete na
kumhakikishia kuwa wanaccm wa mkoa wa Dar es Salaam wako imara na kwamba
wako tayari kwa mapambano ya kisiasa.
Katika tukio jingine, mapema asubuhi, Dr John Pombe Magufuli
akiambatana na mgombea mwenza mama Samia Hassan Suluhu walirejesha na
kusaini fomu za tume ya taifa ya uchaguzi katika mahakama kuu ya
Tanzania kwa mujibu wa taratibu na sheria ya tume hiyo ya taifa ya
uchaguzi ambapo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za tume hiyo wagombea
wote wanahitaji kupata wadhamini wasiopungua mia mbili katika baadhi ya
mikoa ikiwemo visiwa vya Zanzibar.
Post a Comment