Klabu ya Manchester United ambayo msimu huu imedhamiria kupata saini za wachezaji mahiri watakaoweza kurejesha heshima ya kikosi chao kwani toka aondoke Sir Alex Ferguson, klabu hiyo imekuwa na wakati mgumu wa kurudisha makali yake ya awali.
manchester_united_logo_1280x1024
Njia pekee Man United walioamua kuitumia kukijenga upya kikosi chake ni kufanya usajili pekee ndio utakaoweza kuirudisha Man United katika ubora wake, kwa hivi siku za karibuni klabu ya Man United ilikuwa ikihitaji kuipata saini ya beki wa Real Madrid Sergio Ramos na kutumia kigezo cha Real Madrid kumtaka De Gea ili iweze kuwashawishi Real Madrid kumuachia beki huyo.
1420198841_extras_noticia_foton_7_2
Baada ya klabu ya Real Madrid kuweka ngumu na kugoma kumuuza beki huyo kwenda Man United na kumpa mkataba mpya, Man United waliamishia mawazo kwa beki kutokea Ureno anayeitumikia Real Madrid ya Hispania Pepe wakiwa na matumaini ya kumpata, August 21 Real Madrid wametangaza kumsainisha mkataba mpya beki huyo.
124
Pepe ambaye amesaini mkataba mpya utakaomuweka Santiago Bernabeu hadi June 30 2017 alikuwa katika uwezekano wa kuondoka na Man United walikuwa wakimtolea macho kabla Real Madrid kumpa mkataba mpya, Pepe amejiunga na Real Madrid mwaka 2007 akitokea klabu ya FC Porto ya Ureno.

 

Post a Comment