Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge umemalizika kwa Crystal Palace kuharibu rekodi ya Mourinho kutopoteza mechi katika dimba la nyumbani.
Mechi hiyo imemalizika kwa matokeo ya ushindi wa 2-1 kwa Palace inayofundishwa na kocha wa zamani wa Newcastle – Alan Perdew.
Sako alianza kuifungia Palace goli katika dakika ya 65, kabla ya Radamel Falcao kusawazisha katika dakika ya 79.
Dakika ya 81, James Ward aliifungia Palace goli la ushindi na kuzidi kuiharibu rekodi ya Mourinho katika uwanja wa nyumbani ambapo leo alikuwa anatimiza mechi ya 100 tangu alipoanza kuifundisha tena timu hiyo.
Post a Comment