Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekiri kuwa na furaha na kikosi chake cha sasa ila kauli hiyo bado inazua maswali ni kweli hatasajili, ana furaha na kikosi chake? licha ya ofa zake zaidi ya tatu za kuomba kumsajili beki wa kati wa Everton John Stones kukataliwa.
josem_0
Mourinho ambaye ana mchezo mmoja weekend hii dhidi ys Crystal Palace alijibu furaha ya ubora wa kikosi chake licha ya kumkosa John Stones hivyo anaamini ana kikosi bora.
“Huwa sizungumzii wachezaji kutoka timu nyingine nina kikosi bora na nina furaha nacho, kama nitapata nchezaji kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili ni vizuri kama sitapata tutaendelea na wachezaji tuliyonao, nisingependa kufanya kama wengine kuwa namuhitaji Pogba wakati ni mchezaji wa Juventus”>>> Mourinho

Post a Comment