Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambaye mwaka 2013 alikuwa na dhamira ya dhati ya kuwania saini ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Luis Suarez kwa dau la poundi milioni 40, alikuwa yupo tayari kulipa ili Liverpool imuuzie nyota huyo.
Mwaka unaofuatia Liverpool walimuuza Suarez katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania, August 24 Arsene Wenger amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa hawasikitikii Liverpool kumkosa Raheem Sterling kwani hata yeye bado ina muumiza kutouziwa Suarez.
“Liverpool
wapo katika nafasi ambayo wanaweza kufanya maamuzi yao wenyewe,
walikataa kutuuzia Suarez hivyo siwezi kujisikia huzuni sana kwa ajili
yao, binafsi kiwango cha Sterling tutakiona kwa muda mrefu sifikirii
kama Sterling alifanya drama zozote hicho ndicho kilichotokea katika
dirisha la usajili”>>>Sterling
Ikumbukwe kuwa vilabu vingi vya Ulaya
hususani vinavyoshiriki Ligi moja huwa havipendi kuuziana wachezaji
kwani wanaamini hawawezi kukupa silaha halafu uje huwafunge wenyewe.
Hata suala la Peter Cech kujiunga na Arsenal Jose Mourinho alikuwa hajarizia na angependa kuona Peter Cech anacheza nje ya Uingereza.
Post a Comment