Manchester City wambeba Nicolas Otamendi
Manchester City wamemsajili mlinzi wa kimataifa wa Argentina Nicolas
Otamendi kutoka klabu ya Valencia kwa mkataba wa miaka mitano. Mchezaji
huyo mwenye miaka 27 alitajwa katika kikosi bora cha La Liga msimu wa
2014-15 na aliisaidia nchi yake kufika fainali ya Kopa Amerika mwaka
huu. ''Kuwa ndani ya klabu hii kunanifanya ni muhimu sana''alisema
mlinzi huyo wa kati. Meneja wa City Manuel Pellegrini alisema ''Yupo
imara, bora katika kukabiliana na wapinzani na ni bora pia kiufundi''
Post a Comment