Nahodha wa timu ya taifa ya wanawake
ya Uingereza Steph Houghton, Lucy Bronze na mlinda mlango Karen
Bardsley wametajwa katika kikosi bora cha wanawake nyota katika kabumbu.
Wachezaji hao watatu wa klabu ya wanawake ya Manchester City walikua
miongoni mwa wachezaji 23 waliochaguliwa na FIFA katika kikosi hicho.Simba hao wa kike walishinda medali ya shaba wakiwa Canada ngazi bora iliyowahi kufikia timu ya taifa ya wanawake ya Uingereza katika michuano ya kombe la dunia kwa wanawake.
Carli Lloyd aliyefunga mara tatu dhidi ya Japan kwenye michuano hiyo, ni miongoni mwa wachezaji watano kutoka Marekani katika kikosi hicho. Lloyd pia alipata zawadi ya kiatu cha dhahabu kama mchezaji bora wa michuano hiyo.
Post a Comment