Kundi linalofanya kweli kwenye gemu la muziki, Afrika Mashariki la Navy Kenzo.
Boniphace NgumijeKUNDI linalofanya kweli kwenye gemu la muziki, Afrika Mashariki la Navy Kenzo, linaloundwa na wasanii ‘couple’, Aika na Nahreal limezidi kuchana anga baada ya wimbo wao unaoitwa Game kuzidi kufanya vyema kwenye media mbalimbali duniani.
Akichezesha taya na Showbiz, Aika alidai kuwa mafanikio wanayoendelea kuyapata kutokana na wimbo huo waliomshirikisha Vanessa Mdee na video yake kufanywa na produza maarufu Afrika, Justin Compos wa Gorilla Films, ni pamoja na kuuona ukichezwa kwenye media kubwa duniani zikiwemo MTV base, Trace na nyingine kibao.
“Kiukweli wimbo umekuwa mkubwa tofauti na tulivyokuwa tunautegemea, hivi karibuni umeshika namba moja kwenye kituo cha televisheni huko Uingereza, BBC 1xtra wanaucheza lakini pia tumekuwa tukipokea sana simu kutoka kwenye media kubwa, kitu ambacho ni changamoto kwetu kuandaa kazi nzuri tena,” alisema Aika.
Post a Comment