Mgombea urais kupitia UKAWA Mh.Edward Lowassa anatarajia  kuzungumza na makundi mbalimbali ya wanawake kabla ya uzinduzi wa kampeni kwa kueleza mipango alionayo  katika kuinua uchumi wa wanawake na kupambana na umasikini.
Mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Halima Mdee akizungumzana waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema Mh.Lowassa  ambaye ataambatana na mkewe  mama Regina Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali CHADEMA  watazungumza na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya wanawake katika ukumbi wa MILLENIUM  TOWER saa nane mchana mkutano ambao pia  utarushwa moja kwa moja na television ya ITV ambapo Mh.Lowassa atazungumza mikakati alionayo kwa wanawake na watoto na hatma ya maendeleo kwa taifa.
 
Aidha Mdee amesema Mh.Lowassa atapata furs aya kuainisha  kuhusu watoto wa kike wanaokosa fursa za elimu ,sekta ya kilimo ambayo inaajiri wanawake wengi  pamoja na sekta ya afya ambapo pia Bawacha wamegawa kanda kumi  kuhakikisha wanawafikia wanawake katika mikoa yote kupeleka ujumbe wa matumaini kwa wana wake kushiriki harakati z aukombozi kwa taifa lao.
 

Post a Comment