Timu ya Taifa ya wanawake ya TWIGA STARS inatarajiwa kuingia kambini kesho kisiwani ZANZIBAR kujiandaa na Fainali za Michezo ya All Africa Games
ROGASIAN KAIJAGE
Timu ya Taifa ya wanawake ya  TWIGA STARS inatarajiwa kuingia kambini kesho kisiwani ZANZIBAR kujiandaa na Fainali za Michezo ya All Africa Games zitakazofayika nchini CONGO BRAZZAVILE mwezi Septemba mwaka huu.
Kikosi hicho cha wachezaji 25 chini ya Kocha Mkuu ROGASIAN KAIJAGE, tayari kimeanza mazoezi kujiandaa na michuano hiyo ambapo TANZANIA ilikata tiketi ya kushiriki fainali hizo baada ya kuiondoa ZAMBIA kwa jumla ya mabao 6-5.
TWIGA STARS ambayo imefuzu kwa Fainali za Michezo ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi Septemba 04 – 17 imepangwa kundi A na wenyeji CONGO BRAZAVILLE, NIGERIA na IVORY COAST

Post a Comment