Kiongozi wa ofisi ya kisiasa ya kundi la wapiganaji wa TALIBAN huko QATAR, amejiuzulu ikiaminika hatua hiyo ni mgawanyiko ndani ya kundi hilo
SYED MOHAMMAD TAYAB AGHA
Kiongozi wa ofisi ya kisiasa ya kundi la wapiganaji wa TALIBAN huko QATAR, amejiuzulu ikiaminika hatua hiyo ni mgawanyiko ndani ya kundi hilo, kufuatia kifo cha kiongozi wao MULLAH OMAR.
Taarifa iliyotolewa na kiongozi huyo SYED MOHAMMAD TAYAB AGHA, imesema sababu ya kujiuzulu ni hatua ya baadhi ya wafuasi wa kundi hilo kuficha habari za kifo cha MULLAH kilichotokea miaka miwili iliyopita.
Ameongeza kusema TALIBAN inafaa kushughulikia masuala yake yote kutoka AFGHANISTAN, ikiwemo uteuzi wa kiongozi mpya na kwamba ni vigumu kumtumikia kiongozi aliyechaguliwa nje ya AFGHANISTAN.
Taarifa hiyo inadaiwa inamlenga kiongozi mpya MULLAH AKHTAR MANSOUR ambaye alitajwa juma lililopita katika mkutano ulioandaliwa na baraza tawala huko PAKISTAN, huku viongozi wengine wakuu wa TALIBAN wakisema hawakushauriwa katika uteuzi huo.

Post a Comment