Mgombea urais wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch (UKAWA) Mh Edward Lowassa amekamilisha ziara ya kutafuta wadhamini katika visiwa vya Zanzibar na amewaahidi wananchi wa visiwa hivyo kutumia uwezo wake wote kushughulikia kero za muda mrefu zinazowakabili ikiwemo ya muungano ukiukwaji wa haki na wizi wa kura unaofanyika wakati wa uchaguzi.

Akizungumza na wananchi hao katika viwanja vya Kibanda Maiti visiwani Zanzibar Mh Lowassa amesema hatua iliyofikia sasa suala la kuiondoa CCM madarakani halina mjadala kilichobaki ni utekelezaji ambao asilimia kubwa uko mikononi mwa wananchi.
 
Awali makamu wa kwanza wa rais Mh Seiph Sharifu Hamad na mgombea mwenza Mh Duni Haji na mwenyekiti wa chadema Mh Freeman Mbowe  pamoja na kuelezea azima ya UKAWA ya kulinda na kudumisha muungano wamewataka wafanyakazi wa serikali iliyoko madarakani kuacha kuwatisha watendaji hasa wa vyombo vya dola kuwa UKAWA ikiingia madarakani watapoteza ajira zao.



Post a Comment