Kocha mpya wa timu ya Taifa ya soka ya Nigeria Sunday Oliseh amesema kwa sasa yupo tayari kuwaonyesha wale wanaomkosoa kuwa hana uwezo wa kuifanya kazi hiyo
Kocha mpya wa timu ya Taifa ya soka ya Nigeria Sunday Oliseh
Kocha mpya wa timu ya Taifa ya soka ya Nigeria Sunday Oliseh amesema kwa sasa yupo tayari kuwaonyesha wale wanaomkosoa kuwa hana uwezo wa kuifanya kazi hiyo kutokana na kutokuwa na uzoefu.
Oliseh mwenye umri wa miaka 40 mwezi uliopita alisaini kandarasi ya miaka mitatu kuifundisha SUPER EAGLES kuchukua nafasi ya Stephen Keshi alietimuliwa kazi huku baadhi ya wadau wakipinga uteuzi wake kutona na kuwa na uwezo mdogo.
Kocha huyo amesema kama watu wanamkosoa kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kutosha basi wasubiri waone pale atakapoanza kazi huku akihoji kama yeye wanamkosoa je kuna mchezaji yeyote wa zamani toka barani Africa anaefanya kazi ya ukocha barani Ulaya na kama hakuna basi yeye anastahili kupewa kazi hiyo.
Kabla ya kupata kazi hiyo ya kuifundisha SUPER EAGLES, Oliseh alikuwa akifanya kazi ya uchambuzi  wa soka kwenye luninga na mjumbe wa kamati ya ufundi ya FIFA lakini aliwahi kufundisha soka kwenye ngazi ya chini mno nchini Ubelgiji kati ya mwaka 2008 na 2009.
Kibarua cha kwanza cha kocha huyo kitakuwa mwezi Septemba mwaka huu pale timu yake itakapocheza na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Africa ya mwaka 2017 huko nchini Gabon.

Post a Comment