Afrika imekuwa na idadi ndogo sana ya
kupata wachezaji wanaocheza katika Ligi kubwa Duniani lakini wakitokea
mara nyingi huwa wanacheza kwa mafanikio na majina yao kuwa makubwa,
moja kati ya sheria ya mchezaji wa kigeni kucheza katika Ligi Kuu
Uingereza ni lazima nchi yako iwe kunzia nafasi ya 70 kushuka chini
katika viwango vya FIFA au huwe una kipaji kweli au ucheze soka la
ridhaa kwa nchi hiyo ili uweze kupata nafasi.
Nakusogeza na hii Top 10 ya mastaa wa Afrika waliwahi kutamba katika vilabu vya Man City au Chelsea.
10. Emmanuel Adebayor mwaka 2009 ndio ulikuwa uhamisho wake kutoka Arsenal kwenda katika klabu ya Man Ciy
kwa ada ya pound milioni 25 uhamisho ambao ulikuwa pigo kwa Arsenal
kwani Adebayor alikuwa katika kiwango cha juu wakati huo hata mwaka 2008
alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Afrika.
9. Marc-Vivien Foe huyu hadi leo jezi namba 23 haitumiki katika klabu ya Man City
kama heshima kwake, uongozi wa klabu hiyo waliamua kuuistafisha namba
ya jezi hiyo kama heshima kwa mchezaji huyo aliyefia uwanjani June 26
2003 Lyon Ufaransa, hadi anafikwa na umauti Foe alikuwa kiungo muhimu
katika taifa lake Cameroon na klabu ya Man City.
8. John Obi Mikel ni
miongoni mwa wachezaji wachache kutoka Afrika waliojipatia heshima,
umaarufu na mafanikio mengine kutoka katika soka, kiungo huyo wa
kinigeria amepata mafanikio katika klabu Chelsea toka ajiunge nayo mwaka 2006 akiwa chini ya makocha Rafael Benitez, Carlo Ancelotti na Jose Mourinho kwa vipindi tofauti tofauti, amewahi kutwaa mataji 2 ya Ligi Kuu, Kombe la FA 4 na Ligi ya mabingwa Ulaya mara 1 mwaka 2012.
7. Kolo Toure beki wa kati wa Ivory Coast alianza kutengeneza jina lake katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kabla ya kuhamia Man City alihamia Man City alikuwa anaunda safu imara ya ulinzi akishirina na Sol Campbell kabla ya mwaka 2009 kuhamia Man City.
6. Gerem Njitap takwimu zinaonesha amecheza vilabu kadhaa ila Chelsea ni moja kati ya vilabu vyake vikubwa alivyowahi kucheza kwa mafanikio, aina ya uchezaji wake nguvu vilimfanya apendwe sana na Jose Mourinho kama kocha wa Chelsea wakati huo , Gerem
pia amewahi kutwa Kombe la klabu bingwa Ulaya akiwa katika klabu ya
Real Madrid ya Hispania sambasamba na kushinda medali ya dhahabu katika
michuano ya Olympic.
5. Michael Essien amefanya vizuri sana na klabu ya Chelsea amewahi kucheza vilabu mbalimbali kabla ya kutua Chelsea
ni miongoni mwa viuongo bora na wenye nguvu kutoka katika bara la
Afrika majeraha ya goti yasiomuisha yamemfanya kukosa na namba katika
klabu ya Chelsea licha awali alikuwa ana mchango mkubwa sana Stamford Bridge.
4. Didier Drogba amefanya vizuri sana na Chelsea kiasi hata cha kuweka rekodi ya kuwa ni mchezaji mwenye rekodi ya aina yake kwani kuna kipindi ilikuwa kila anapokutana na Arsenal ni lazima afunge goli, yupo katika list ya wachezaji wenye heshima zaidi katika historia ya klabu ya Chelsea lakini pia sambamba na Afrika ana nafasi kubwa sana katika soka na kuitangaza Afrika.
3. Yaya Toure alitokea katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania na kujiunga na klabu ya Man City ya Uingereza alifanya vizuri akiwa na FC Barcelona
licha ya kuwa jina lake halikuwa likitajwa sana kutokana na kikosi
hicho kusheheni majina ya wachezaji wazuri na wenye uwezo sana kama Lionel Messi ni muhimili mkubwa sana katika safu ya kiungo kwa klabu yake na taifa lake Ivory Coast.
2. George Weah
huyu ni mchezaji mwenye historia ya kipekee barani Afrika kwani ndiye
mchezaji pekee kutoka bara hili kuwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa
Dunia (Ballon d’Or) aliwahi kufanya hivyo mwaka 1995 akiwa katika klabu
ya AC Milan ya Italia, amewahi kutamba pia katika klabu ya Man City lakini ndiye mchezaji pekee wa Afrika aliyecheza vilabu vyote viwili Man City na Chelsea.
1. Samuel Eto’o ni kama George Weah alihamia Chelsea
katika nyakati ambazo alikuwa anatajwa kumazia muda wake wa kucheza
kutokana na umri wake hakuwahi kufanya makubwa sana na klabu hiyo kwa
muda mfupi aliokaa klabuni hapo ila magoli matatu aliowafunga Man United hayatasahaulika kamwe kwani ulikuwa ndio wakati ambao kejeli za Eto’o
kuitwa mzee zilitawala, amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika
mara nne ni mchezaji pekee wa Afrika aliewahi kutwa Kombe la Ligi ya
Mabingwa Ulaya mara tatu.
Post a Comment