Wazee wa CHADEMA wampongeza Kingunge

Ikiwa ni siku chache tangu kada wa chama cha mapinduzi CCM Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ajionoe katika chama hicho baadhi ya wazee wamempongeza.

Miongoni mwa wazee waliojitokeza na kutoa pongezi hizo ni pamoja na wale wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA ambao wamempongeza kada huyo kwa uamuzi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee CHADEMA, Roderick Lutembeka amesema, wamelazimika kutoa pongezi hizo kutokana na maneno ya Mzee Kingunge kuwa ya busara na yenye kutaka kulipeleka taifa kwenye maendeleo.

 

Post a Comment